Wednesday, January 17, 2007

Chapisho


MIAKA 2000 YA UKRISTO: HISTORIA ILIYOPOTOSHWA
Katika kitabu hiki, nimeeleza mambo mengi ya uongo yanayofundishwa na makanisa. Kwa hakika yaliyokuwa yameaminiwa tangu zamani za kale huenda yakawa ya uongo.Kitabu hiki kimeelezea mambo mengi—ikiwamo Krismasi—ambayo yanaheshimiwa na Ukristo lakini si ya Kikristo. Kwa kusoma kitabu hiki utagundua kuwa mambo yote yanayotendeka nyakati za Krismasi yanathibitisha kwamba Krismasi si ya Kikristo bali ni ya kipagani. Lazima iwe wazi kwamba Krismasi ni sherehe ya kipagani, upagani hadi katika kiini chake, na katika hali zote Krismasi ina vidokezo vyote vya kipagani, umuhimu wote wa kipagani na maana zake zilizofichika za kipagani.Pia itawashangaza sana kwa watu kutambua kuwa kushurutisha mapadri na makasisi kutooa ni mafundisho ya mashetani yanayofundishwa na makanisa. Kristo na Mitume wake hawakudai halidai useja wa kushurutishwa kwa wahudumu wa kanisa. Yesu mwenyewe hakuweka jambo hilo kama sharti la kuwachagua Mitume wake Kumi na Wawili, wala Mitume walioongoza Ukristo katika zile siku za mwanzo hawakuwalazimisha watu wasioe ili wawe watumishi. Kwanini leo makanisa yanashurutisha jambo ambalo Biblia haishurutishi? Majibu haya na mengine mengi utayapata katika kitabu hiki: MIAKA 2000 YA UKRISTO: HISTORIA ILIYOPOTOSHWA.

No comments: