Damu ya makumi ya maelfu ya wanadamu wasio na hatia ilimwagika katika kipindi cha miaka kumi tangu 2001 hadi 2011 kwa kile kinachodaiwa kuwa ni ‘ugaidi’ na VITA DHIDI YA UGAIDI. Katika mwaka wa kumi wa vita hivyo, Marekani ikadai kuwa imemuua kiongozi wa mtandao wa kigaidi wa al-Qaeda, Osama bin Laden, ambaye wanadai kuwa ndiye aliyeandaa ugaidi dhidi ya Marekani Septemba 11, 2001. Ukweli ni kwamba waliohusika na ‘ugaidi’ huo hawakutajwa, na waliotajwa hawakuhusika. Osama bin Laden hakuhusika kwa vyovyote na ugaidi huo dhidi ya Marekani. Hata hivyo, kifo chake nacho kina utata mwingi. Mengi yaliyosemwa ni ya kutungwa kwa kusudi la kuihadaa dunia. Mengi, au yote, yaliyodaiwa kuithibitishia dunia kuwa Osama bin Laden alikuwa na hatia ya kufanya ugaidi huo ni ushahidi wa bandia. Mwandishi wa Hadaa ameweka wazi uchambuzi wa tafiti zilizofanywa kuhusu ugaidi huo ulioitikisa dunia na udanganyifu uliotawala tukio hilo na mazingira ya ‘kifo’ cha Osama bin Laden.
Ikiwa msomaji atavumilia na kukisoma kitabu hiki hata ukurasa wa mwisho, huenda imani yake katika mambo mengi kuhusu tukio la Septemba 11, 2001 na ‘kuuawa’ kwa Osama bin Laden Mei 2011 ikabadilika moja kwa moja.
Kitabu hicho kimechapishwa mwishoni mwa Julai 2011
No comments:
Post a Comment